Page 84 - Jiografia_Mazingira
P. 84
Kwa ujumla, unapotumia ramani, ili kutambua sura ya nchi katika
eneo fulani, zingatia rangi au mistari ya kontua. Kuelewa sura ya
nchi ni muhimu kwa sababu mbalimbali, kama vile kuchagua eneo
la ujenzi na kufahamu kuhusu mazingira.
Kazi ya kufanya namba 10
FOR ONLINE READING ONLY
Chunguza Kilelezo namba 28, kisha jibu maswali yanayofuata:
Kielelezo namba 28: Sura ya nchi katika Wilaya ya Karatu
Maswali
1. Baini maumbo ya sura ya nchi yaliyomo katika ramani.
2. Shughuli gani za kiuchumi zinazoweza kufanyika katika
maumbo ya sura ya nchi uliyoyabaini.
3. Bainisha alama zilizotumika katika ramani kuwakilisha maumbo
ya sura ya nchi.
77
31/10/2024 19:19
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 77
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 77 31/10/2024 19:19