Page 83 - Jiografia_Mazingira
P. 83
Maswali
1 Ni mipaka ipi ya kiutawala imebainishwa katika ramani?
2 Eleza tofauti ya mipaka ya mkoa na mipaka ya wilaya
iliyobainishwa katika kielelezo namba 27.
FOR ONLINE READING ONLY
3 Ni athari gani za kijamii na kiuchumi zinazoweza kutokea
kutokana na kushindwa kubaini mipaka ya kiutawala kwa
usahihi?
Kutumia ramani kubaini maumbo ya sura ya nchi
Sura ya nchi inarejelea jinsi ardhi inavyoonekana, kama vile milima,
mabonde na maeneo ya tambarare. Ramani hutumia alama au
rangi tofauti kuonesha sura ya nchi. Kwa mfano, alama ya mistari
ya kontua kwenye ramani hutumika kuonesha jinsi eneo lilivyoinuka
au kudidimia.
Milima na vilima
Mara nyingi, milima na vilima huoneshwa kwa rangi ya kahawia au
nyekundu au kwa mistari ya kontua. Kadiri rangi inavyokolea, ndivyo
mlima ulivyo mrefu zaidi. Au, iwapo mistari ya kontua imekaribiana
sana, ina maana kuwa ardhi ina mteremko mkali kama vile mlima.
Vilima, ambavyo ni vidogo kuliko milima, huoneshwa kwa rangi ya
kahawia isiyokolea au kijani, au kwa mistari ya kontua iliyokaribiana
kiasi.
Mabonde na maeneo tambarare
Mabonde ni maeneo ya chini katikati ya milima au vilima. Katika
ramani huoneshwa kwa rangi ya kijani au mistari ya kontua iliyopinda
kuelekea ndani. Maeneo tambarare, mara nyingi huoneshwa kwa
rangi ya kijani. Pia, yanaweza kuwakilishwa na mistari ya kontua.
Ikiwa mistari iko mbalimbali, inamaanisha kuwa ardhi ni tambarare.
Uwanda wa juu
Haya ni maeneo yaliyoinuka yenye sehemu tambarare juu yake,
ambayo kwa kawaida huoneshwa kwa rangi ya kahawia. Pia,
katika ramani uwanda wa juu unaweza kuoneshwa kwa mistari ya
kontua iliyokaribiana pembeni na iliyosambaa kwa juu yake. Mistari
iliyosambaa inaonesha sehemu tambarare ya uwanda wa juu.
76
31/10/2024 19:19
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 76
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 76 31/10/2024 19:19