Page 85 - Jiografia_Mazingira
P. 85
Kutumia ramani kubaini mtawanyiko wa vitu na watu
Kazi ya kufanya namba 11
Tumia vitabu au vyanzo vya kuaminika vya mtandaoni,
FOR ONLINE READING ONLY
soma kuhusu namna mtawanyiko wa watu na vitu unavyoweza
kuwakilishwa katika ramani
Ramani ni zana muhimu inayoweza kutumika kubaini mahali ambapo
watu wanaishi na vitu tofauti vinapatikana. Ramani zinaweza kutumia
alama ya vidoti au rangi kuonesha idadi au mtawanyiko wa watu.
Kwa mfano, ikiwa kwenye ramani unaona doti nyingi zilizokaribiana,
inamaanisha kuwa kuna watu wengi wanaishi katika eneo hilo,
mfano katika miji mikubwa. Iwapo doti zimesambaa, inamaanisha
eneo hilo lina watu wachache, mfano kiijijini au kwenye miji midogo.
Pia, unaweza kubaini mtawanyiko wa watu na vitu kwa kutumia
mifumo ya taarifa za kijiografia (GIS) na zana nyingine za kidijitali.
Hii inatusaidia kuelewa maeneo yenye watu wengi zaidi au kidogo.
Vilevile, ramani hutumia alama mahususi kuonesha mtawanyiko
wa vitu tofauti juu ya uso wa dunia. Kwa mfano, alama ya nyumba
inaonesha mahali ambapo nyumba zinapatikana, wakati alama ya
shule inaonesha mahali ambapo shule zinapatikana. Ramani pia
hutumia rangi tofauti kuonesha maeneo. Kwa mfano, buluu inaweza
kutumika kuonesha vyanzo vya maji kama mito na maziwa, kijani
kwa maeneo yenye misitu au uoto, na njano kwa eneo lenye jangwa.
Kwa ujumla, unashauriwa kutumia ufunguo ili kuona ni alama gani
au rangi gani zimetumika kuwakilisha mtawanyiko wa vitu na watu
ili uweze kutumia ramani vizuri.
78
31/10/2024 19:19
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 78
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 78 31/10/2024 19:19