Page 72 - Jiografia_Mazingira
P. 72
Maswali
Kwa kutumia rula;
(a) Kokotoa umbali wa kutoka Kitunda Misioni mpaka ofisi ya
kijiji.
FOR ONLINE READING ONLY
(b) Kokotoa umbali wa kutoka ofisi ya kijiji mpaka ofisi ya
kitongoji.
(c) Kokotoa umbali wa kutoka ofisi ya kitongoji mpaka Kitunda
Misioni.
Upimaji wa umbali usionyooka
Ili kupima umbali wa vitu visivyonyooka kama vile mto, barabara au
reli, vifaa kama bikari, kipande cha karatasi, uzi na skeli ya ramani
hutumika.
1. Kutumia uzi
Zifuatazo ni hatua za kubaini umbali usionyooka katika ramani kwa
kutumia uzi.
(a) Baini vituo viwili vinavyounganika kwa mstari usionyooka.
Kwa mfano, kituo A na B, kisha gawa umbali unaohitajika
kupimwa katika vipande vifupivifupi ambavyo vimenyooka na
weka alama kama inavyoonekana katika Kielelezo namba 13.
Kielelezo namba 13: Umbali unaohitajika kupimwa kutoka kituo A hadi kituo B
(b) Chukua uzi na ufunge fundo kwenye ncha ya mwisho upande
wa kushoto, kisha ulaze uzi huo kwenye mstari usionyooka
unaounganisha vituo viwili kwakufuatisha vipande vifupivifupi
ulivyovigawa katika mstari, na weka alama kwenye uzi huo
kuelekea upande wa pili. Funga fundo la pili kwenye uzi
65
31/10/2024 19:19
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 65
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 65 31/10/2024 19:19