Page 27 - Jiografia_Mazingira
P. 27
kwenye ramani, dira na nyenzo mbalimbali za usafiri ili kusaidia
kufahamu eneo mahususi lilipo na uelekeo wa kulifikia eneo hilo.
Aidha, Pande Kuu za Dunia zinaunda msingi wa pande nyingine
zaidi za dunia.
FOR ONLINE READING ONLY
Kazi ya kufanya namba 1
Fuata hatua zifuatazo kuchora mchoro wa Pande Kuu
za Dunia.
(a) Nenda nje ya chumba cha darasa wakati wa asubuhi;
(b) chora duara mahali uliposimama;
(c) baini Jua linakochomoza na geukia upande huo;
(d) tembea hatua tatu mbele kuelekea upande wa jua linakochomoza,
simama na uandike neno Mashariki (Mas);
(e) rudi kwenye duara ukiendelea kutazama Jua linakochomoza,
kisha tembea hatua tatu kurudi nyuma, simama na andika
neno Magharibi (Magh);
(f) rudi tena kwenye duara huku ukiendelea kuangalia upande
wa Jua;
(g) geuka mkono wa kulia, tembea hatua tatu kisha andika neno
Kusini (Kus);
(h) rudi tena kwenye duara na uangalie Jua linakochomoza.
Kisha, geuka kushoto na utembee hatua tatu mbele na
uandike neno Kaskazini (Kas);
(i) chukua kijiti na uchore mistari iliyonyooka kutoka kwenye
kila neno uliloandika ardhini kuelekea kwenye duara; na
(j) Chunguza mchoro huo kisha uchore kwenye daftari lako.
20
31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 20 31/10/2024 19:18
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 20