Page 10 - Jiografia_Mazingira
P. 10
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 1: Topografia ya Mkoa wa Tanga
Ramani za kisiasa
Ramani hizi zinatoa taarifa kuhusu mipaka ya nchi, mikoa, wilaya na
maeneo mengine ndani ya nchi. Pia, zinaonesha maeneo muhimu
kama vile: majengo ya serikali, pamoja na miji mikuu au muhimu,
kama inavyoonekana katika Kielelezo namba 2. Ramani za kisiasa
ni muhimu kwa watafiti, wanafunzi na wageni wanaohitaji kuelewa
mipaka ya kiutawala ya eneo fulani.
Ramani za kisiasa huweza kubadilika baada ya muda fulani. Baadhi
ya mambo yanayoweza kusababisha mabadiliko kwenye ramani za
kisiasa ni pamoja na vita, migogoro ya mipaka kati ya nchi na nchi,
kuundwa kwa taifa jipya, makubaliano ya kisiasa, na mabadiliko
ya mipaka ndani ya nchi. Kwa sababu ya mambo haya, ramani za
kisiasa huchorwa upya ili kuonesha muonekano wa sasa wa nchi
au eneo husika.
3
31/10/2024 19:17
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 3
JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd 3 31/10/2024 19:17