Page 143 - SayansiStd4
P. 143

3.  Bloku ya ‘zunguka digrii 15 Q/nyuzi’ kinyume cha mwelekeo
                    wa mshale wa saa hutekelezwa kabla ya bloku ya ‘ikiwa
                    kwenye ukingo wa jukwaa, rejesha’.


              4.  Bloku ya  ‘ikiwa kwenye ukingo wa jukwaa, rejesha’
          FOR ONLINE READING ONLY
                    huchezwa mwishoni.


















                            Kielelezo namba 33: Mlolongo katika usimbaji
              Hivyo, mtiririko huu unakuwa kama ifuatavyo:


              ‘Wakati  inapobonyezwa’  →  ‘enda kwa (mahali popote)’  →
              ‘zunguka 15 digrii/nyuzi’ → ‘ikiwa kwenye ukingo wa jukwaa,
              rejesha’.


              Muundo wa marudio katika usimbaji

              Katika uundaji wa programu za kompyuta,  unaweza kuhitaji
              jambo  fulani lijirudie mara  kadhaa.  Kwa mfano, unaweza

              kuhitaji mwendo au sauti ijirudie bila wewe kubofya kitufe cha
              ‘Anza’. Uwezo huo katika usimbaji unajulikana kama marudio.
              Unapotumia  marudio,  unaiamuru  kompyuta kurudia  jambo
              fulani mara nyingi kadiri unavyotaka.



                 Kazi ya kufanya namba 11: Mchezo wa sauti unaojirudia



               Unaweza kucheza sauti kwa kuifanya ijirudie kulingana na
               idadi  unayotaka. Hatua zifuatazo zitakuongoza  kuunda
               mchezo unaorudia sauti mara nyingi.




                                                   136



                                                                                            14/01/2025   18:39
     SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd   136
     SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd   136                                  14/01/2025   18:39
   138   139   140   141   142   143   144   145   146   147   148