Page 142 - SayansiStd4
P. 142
4. Baada ya kuunganisha utapata programu kama
inavyooneshwa katika Kielelezo namba 32.
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 32: Bloku ya ‘cheza sauti’ imeunganishwa na bloku
ya ‘wakati inapobonyezwa’
5. Bofya ‘Anza’ kucheza mchezo na usikilize sauti inayotoka.
Umesikia nini ulipocheza?
Miundo ya kudhibiti programu
Miundo ya kudhibiti programu inahusu jinsi mtiririko wa
maelekezo ya kompyuta unavyodhibitiwa. Kuna aina tatu
za miundo ya kudhibiti programu. Miundo hiyo ni mlolongo,
marudio na maamuzi.
Muundo wa mlolongo katika usimbaji
Katika usimbaji, programu huenda katika mtiririko ambao
hufuata namna bloku zilivyopangwa. Bloku ya kwanza
inatekelezwa kabla ya bloku inayofuata. Kwa mfano, katika
Kielelezo namba 33:
1. Bloku ya ‘wakati inapobonyezwa’ hutekelezwa kabla ya
bloku ya ‘enda kwa (mahali popote)’.
2. Bloku ya ‘enda kwa (mahali popote) ‘ hutelekezwa kabla
ya bloku ya ‘zunguka digrii/nyuzi’.
135
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 135
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 135 14/01/2025 18:39