Page 137 - English_F5
P. 137
English
Baada ya kugundua nina sifa zote zilizoorodheshwa kwenye tangazo, niliamua kutuma
barua ya maombi kwa kuambatanisha na wasifu wangu, vyeti vya taaluma na cheti cha
kuzaliwa. Kila siku nilikuwa ninapitia tovuti ya shule ili kujua kama kuna taarifa mpya.
Baada ya wiki mbili kupita, niliona jina langu miongoni mwa majina 20 ya waombaji
walioitwa kwenye usaili kwa ajili ya somo la Kiingereza. Nilianza kujiandaa huku
nikiwa na hofu sana kwani sikuwahi kuhudhuria usaili hapo kabla.
FOR ONLINE READING ONLY
Baada ya kuona nina hofu sana, mama aliniambia, “Jiamini mwanangu. Utafanya vizuri
tu maana uwezo wako ni mkubwa. Endelea kufanya maandalizi.” Hofu ikapungua kwa
sababu kauli ya mama ilinipa motisha. Siku ya usaili ilipofika, niliamka alfajiri sana
na kujiandaa. Kabla sijaondoka nyumbani, mama alinitakia kila la kheri huku akisali
kwa ajili yangu. Tulipokuwa eneo la usaili, tuliitwa mmoja baada ya mwingine kwenda
kufanyiwa usaili. Zamu yangu ilipokaribia, nikaanza kutetemeka mwili mzima huku
nikimuomba mwenyezi Mungu anipe ujasiri. Nashukuru Mungu alijibu maombi yangu
kwani nilivyoitwa nikapata nguvu, ujasiri mkubwa na nilijiamini sana. Nilijibu maswali
yote kwa ufasaha mkubwa. Baada ya mwezi mmoja, makamu mkuu wa shule alinipigia
simu kunijulisha kuwa nilifaulu usaili hivyo nikaripoti kazini ndani ya wiki mbili.
Machozi ya furaha yalinidondoka maana ushindani ulikuwa mkubwa sana. Sitaweza
kuisahau siku hiyo katika maisha yangu.
(e) Compare your interpretation with those of your fellow students by considering the
following: Knowledge of the language, concentration and memory, multi-tasking
skills, accuracy (correctness), clarity of information presentation, consistency,
grammar, punctuation, fluency (whether the ideas flowed naturally and carried
the sense and atmosphere of the original work), and whether they elicited the same
emotional response in the listeners as the original.
(f) Imagine you are in a restaurant having breakfast. Suddenly, a foreigner enters and
is seated next to you to have breakfast. Unfortunately, she struggles to place her
order as she cannot communicate in Kiswahili. She speaks only English whereas
the waitress can communicate in Kiswahili only. Given your excellent command of
both languages, you decide to interpret the conversation between the parties in both
directions. Role-play this scenario, with you being the interpreter. The following is
the conversation.
Foreigner: Hello, how’re you this morning?
Interpreter:
Waitress: Nzuri. Vipi, wewe mzima?
Interpreter:
Foreigner: I’m fine too.
Interpreter:
Form Five 128 Tanzania Institute of Education (TIE)
24/06/2024 22:26
ENGLISH FORM 5.indd 128 24/06/2024 22:26
ENGLISH FORM 5.indd 128