Page 91 - Jiografia_Mazingira
P. 91

Jaribio

          Sehemu A: Chagua herufi ya jibu sahihi

          1.  Lengo kuu la ramani ni nini?

             (a) Kuonesha jinsi ya kuchora picha.
        FOR ONLINE READING ONLY
             (b) Kuonesha mahali vitu vilipo katika uso wa Dunia.

             (c)  Kuonesha jinsi ya kukokotoa umbali.

             (d) Kuonesha njia za uokoaji.

          2.  Kabla ya kuchagua ramani kwa mahitaji yako, ni swali gani
             muhimu unapaswa kujiuliza?

             (a) Ramani hiyo imetumia skeli gani?

             (b) Lengo la ramani hiyo ni nini?

             (c)  Ramani hiyo ina rangi gani?

             (d) Ramani hiyo ni kubwa kiasi gani?
          3.  Kipengele gani muhimu cha ramani kinaweza kutumika kubaini

             umbali halisi kwenye ardhi?

             (a) Funguo.

             (b) Skeli.

             (c)  Kichwa cha ramani.
             (d) Mstari wa Gridi.

          4.  Sifa gani ya ramani inahakikisha kwamba taarifa iliyooneshwa

             ni sahihi?

             (a) Inapaswa kutumia rangi angavu na maandishi safi na wazi.

             (b) Inapaswa kuwa na taarifa za hivi punde.
             (c)  Inapaswa kuwa rahisi kusoma na kutafsiri.

             (d) Inapaswa kuwa na kichwa cha ramani.

          5.  Kwa nini ni muhimu kwa ramani kutumia alama, rangi, na mitindo
             sawa kwa ramani nzima?





                                                 84



                                                                                          31/10/2024   19:19
   JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd   84                                           31/10/2024   19:19
   JIOGRAFIA NA MAZINGIRA DARASA LA 4.indd   84
   86   87   88   89   90   91   92   93   94   95   96