Page 76 - SayansiStd4
P. 76
Tahadhari: Unapaswa kuchukua tahadhari wakati
unapofanya jaribio hili.
Hatua
FOR ONLINE READING ONLY
1. Panga kuni katika eneo la wazi uliloliandaa.
2. Washa kuni hizo kwa kutumia majani makavu au vipande
vya karatasi.
3. Chochea kuni hadi ziteketee kabisa.
4. Chunguza nini kimetokea baada ya kuni kuungua.
Matokeo
Jaribio lilifanyika katika mazingira ya wazi ili kuhakikisha
kunakuwa na oksijeni ya kutosha kusaidia kuni kuungua na
kuteketea kabisa. Kuni zilipowashwa kwa kutumia majani
makavu au vipande vya karatasi, zilishika moto na kuanza
kuungua. Kadri kuni zilivyoendelea kuungua, mwali mkali wa
moto ulionekana. Baada ya kuni kuungua kabisa, kilichosalia
ni majivu pekee. Kuchoma kuni au mkaa wakati wa kupika ni
mfano wa uunguaji kamili.
Hitimisho
Jaribio linathibitisha uunguaji kamili, kwani kuni ziliungua
kabisa na kuwa majivu kutokana na uwepo wa oksijeni ya
kutosha.
Uunguaji usio kamili
Uunguaji usio kamili hutokea wakati fueli inapowaka katika
kiasi kidogo cha gesi ya oksijeni.
69
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 69
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 69 14/01/2025 18:39