Page 77 - SayansiStd4
P. 77
Jaribio namba 3: Kuchunguza uunguaji usio kamili
Lengo: Kuonesha uunguaji usio kamili
FOR ONLINE READING ONLY
Mahitaji: Kuni, majani makavu au vipande vya karatasi,
chanzo cha moto, chombo kikubwa cha chuma,
eneo la wazi, na kifaa cha kutifulia udongo.
Hatua
1. Panga kuni kwenye eneo la wazi uliloliandaa.
2. Washa kuni moto kwa kutumia majani makavu au
karatasi.
3. Chochea moto hadi kuni zishike moto kisawasawa.
4. Funika moto kwa chombo cha chuma ulichokiandaa.
5. Funika sehemu zote zinazoweza kuingiza hewa kwa
kutumia udongo.
6. Subiri kwa muda wa usiku mmoja kisha ufunue.
7. Andika matokeo ya uchunguzi.
Maswali
1. Andika tofauti kati ya matokeo ya jaribio namba 2 na
jaribio namba 3.
2. Nini kilisababisha tofauti hizo?
Matokeo
Kuni zikichomwa katika kifaa maalumu kinachozuia
upatikanaji wa oksijeni kunasababisha uunguaji usio kamili.
Baada ya kufunua kifaa hicho siku iliyofuata, ilionekana kuwa
kuni hazikuungua na kuteketea kabisa, hali inayoashiria
uunguaji usio kamili.
70
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 70
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 70 14/01/2025 18:39