Page 75 - SayansiStd4
P. 75
4. Chunguza matokeo kwa mishumaa yote kwa muda wa
dakika moja.
5. Andika matokeo ya uchunguzi uliyoyaona kwa kila
FOR ONLINE READING ONLY
mshumaa.
Swali
Andika sababu za matokeo ya uchunguzi.
Matokeo
Mshumaa A uliendelea kuwaka kwa sababu kuna oksijeni ya
kutosha kusaidia vitu kuwaka. Mshumaa B ulikuwa unaungua
polepole na hatimaye kuzimika kutokana na ukosefu wa
oksijeni ya kutosha.
Hitimisho
Jaribio linaonyesha kwamba oksijeni ni muhimu katika
uunguaji wa vitu.
Aina za uunguaji
Kuna aina mbalimbali za uunguaji wa vitu. Miongoni mwa aina
hizo ni pamoja na uunguaji kamili na uunguaji usio kamili.
Uunguaji kamili
Uunguaji kamili hutokea wakati fueli inapowaka kwenye uwepo
wa gesi ya oksijeni ya kutosha.
Jaribio namba 2: Kuchunguza uunguaji kamili
Lengo: Kuonesha uunguaji kamili
Mahitaji: Kuni, majani makavu au vipande vya karatasi,
chanzo cha moto na eneo la wazi
68
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 68
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 68 14/01/2025 18:39