Page 70 - SayansiStd4
P. 70
5. Maji yakipata joto huchemka na kubadilika kuwa _____.
(a) mvuke
(b) maziwa
FOR ONLINE READING ONLY
(c) barafu
(d) kimiminika
Sehemu B: Andika KWELI kwa sentensi sahihi na SI KWELI
kwa sentensi isiyo sahihi.
6. Maji yaliyopatikana kwa kupoza mvuke wa maji ni safi
na salama.
7. Mara nyingi mvua ya mawe hutokea katika mazingira
yenye jotoridi la chini sana.
8. Maji yaliyochemshwa na kufikia kizingiti cha mchemko
wa maji ni salama kwa kunywa.
9. Chakula kilichogandishwa kinaweza kudumu kwa muda
mrefu bila kuharibika.
10. Wakati maji yanaganda, hubadirika kuwa gesi mara
moja.
Sehemu C: Maswali ya majibu mafupi
11. Eleza namna unavyoweza kubadili maji kuwa mvuke na
kutoka mvuke kurudi katika hali ya kimiminika (maji).
12. Unawezaje kutumia maji yakiwa katika hali ya yabisi,
kimiminika na gesi?
13. Eleza umuhimu wa kizingiti cha mgando wa maji na
kizingiti cha mchemko wa maji.
14. Tofautisha sifa ya maji katika hali yabisi, kimiminika na
gesi.
63
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 63 14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 63