Page 67 - SayansiStd4
P. 67
Endelea kupima jotoridi hadi barafu inapoanza kutokea.
Rekodi uchunguzi ulioufanya.
5. Linganisha jotoridi la maji katika hali yabisi na hali ya
FOR ONLINE READING ONLY
kimiminika.
Matokeo
Maji yanapofikia jotoridi la nyuzijoto sentigredi 0 (nyuzijoto
farenhaiti 32), huanza kuganda. Hivyo basi, maji huganda
katika joto maalum linalojulikana kama kizingiti cha mgando
wa maji. Kizingiti cha mgando wa maji, ambacho ni nyuzijoto
sentigredi 0 (nyuzijoto farenhaiti 32), ni jotoridi maalumu
ambapo maji hubadilika kutoka hali ya kimiminika na kuwa
hali ya yabisi (barafu).
Hitimisho
Jaribio hili linathibitisha kwamba kizingiti cha mgando wa maji
ni nyuzijoto sentigredi 0 (nyuzijoto farenhaiti 32), ambapo
maji huanza kubadilika kutoka hali ya kimiminika na kuwa
hali ya yabisi (barafu).
Kizingiti cha mchemko wa maji
Maji huchemka yanapofikia jotoridi maalumu. Kizingiti cha
kuchemka ni jotoridi maalumu ambapo kimiminika (maji)
huchemka na kubadilika kuwa mvuke. Kizingiti cha mchemko
wa maji ni muhimu kwa sababu tunapata maji salama ya
kunywa. Vilevile, baadhi ya vyakula huiva vizuri pale ambapo
maji yamechemka kufikia jotoridi hilo.
60
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 60
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 60 14/01/2025 18:39