Page 64 - SayansiStd4
P. 64
4. Chukua kioo weka mbele ya mdomo wa birika; Kielelezo
namba 4 kinaonesha kubadilisha gesi kuwa kimiminika.
5. Chunguza kinachoonekana kwenye kioo. Eleza matokeo
FOR ONLINE READING ONLY
ya uchunguzi.
Kielelezo namba 4: Kubadilisha gesi kuwa kimiminika
Matokeo
Kimiminika (maji) yanapochemka, mvuke hutoka kupitia
mdomo wa birika. Mvuke unapogusa uso wa kioo au glasi
wenye jotoridi la chini, hukusanyika na kuwa matone madogo
ya maji. Hii inaonyesha kwamba mvuke (gesi) unapopozwa
hubadilika kuwa kimiminika (maji).
Hitimisho
Jaribio linaonyesha mchakato wa kubadilisha mvuke kuwa
hali ya kimiminika (maji) kupitia mchakato wa utoneshaji.
Maji yanaweza kuwa katika hali mbalimbali, kama vile yabisi,
kimiminika, na gesi. Joto la maji likishuka chini ya nyuzijoto
sentigredi 0 (nyuzijoto farenhaiti 32), yanageuka kuwa hali
ya yabisi inayoitwa barafu. Joto likipanda juu ya nyuzijoto
57
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 57
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 57 14/01/2025 18:39