Page 63 - SayansiStd4
P. 63
Matokeo
Jotoridi linapoongezeka kufikia nyuzijoto sentigredi 100 maji
huchemka na hutoa mvuke ambao ni maji katika hali ya gesi.
FOR ONLINE READING ONLY
Maji katika hali ya gesi hayana rangi, harufu, umbo au ujazo
maalumu wala hayashikiki. Pia husambaa kujaza nafasi
yoyote iliyo wazi. Mvuke unapopozwa, hubadilika tena na
kuwa kimiminika (maji).
Hitimisho
Jaribio linaonesha kwamba maji katika hali yake ya gesi
hayana umbo maalum wala ujazo maalumu, na yanapopozwa
hubadilika tena kuwa kimiminika (maji).
Jaribio namba 4: Kubadilisha gesi kuwa hali ya kimiminika
Lengo: Kuonesha mabadiliko ya gesi kuwa hali ya
kimiminika
Mahitaji: Kioo, glasi, maji, birika na chanzo cha moto
(jiko)
Hatua
1. Weka maji kwenye birika.
2. Washa jiko, kisha weka birika yenye maji kwenye jiko.
Acha yaanze kuchemka.
3. Chunguza kinachoonekana kwenye mdomo wa birika
maji yanapoanza kuchemka.
56
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 56 14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 56