Page 59 - SayansiStd4
P. 59
Gesi
Gesi haina umbo maalumu na ni nyepesi zaidi kuliko yabisi na
kimiminika. Mfano wa gesi ni hewa. Hewa hutunzwa katika vitu
yabisi. Kielelezo namba 3 kinaonesha maputo yenye hewa.
FOR ONLINE READING ONLY
Kadiri hewa inavyojazwa kwenye maputo, ukubwa wa maputo
huongezeka.
Kielelezo namba 3: Maputo yenye hewa
Kuchunguza sifa za maada
Maada inaweza kubadilika kutoka hali moja kwenda hali
nyingine. Hali za maada zinategemea mabadiliko ya jotoridi.
Majaribio namba 1-4, yatatumika kuonesha hali tatu za maada
kwa kutumia maji.
Jaribio namba 1: Kuchunguza sifa za maji katika hali yabisi
Lengo: Kuonesha tabia za maji katika hali yabisi
Mahitaji: Vipande sita vya barafu vyenye ukubwa sawa,
sufuria, deli la kutunzia barafu, kitu chenye
uso ulionyooka kama vile sinia, jagi na jiko au
chanzo chochote cha moto
52
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 52
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 52 14/01/2025 18:39