Page 56 - SayansiStd4
P. 56
7. Je, ni kwa namna gani wadudu kama nzi, mende na mbu
ni hatari kwa afya ya binadamu?
8. Unaweza kufanya nini ili kupunguza kuzaliana kwa nzi
FOR ONLINE READING ONLY
karibu na nyumba yenu?
Msamiati
Lava funza aliye katika hatua ya pili ya
ukuaji wa nzi baada ya yai kuanguliwa
Malengelenge uvimbe wenye majimaji unaotokea
kwenye ngozi
Magonjwa nyemelezi magonjwa mbalimbali ya mara kwa
mara yanayompata mtu mwenye
upungufu wa kinga mwilini
Mzio hali ya mwili kuathiriwa na baadhi ya
vitu ambavyo havileti madhara kwa
watu wengine. Vitu hivyo ni kama vile
vumbi, chavua na harufu
Vimelea viumbehai visivyoonekana kwa macho
vinavyosababisha magonjwa
Virusi vimelea vidogo sana visivyoonekana
kwa macho ya kawaida ambavyo
huzaliana ndani ya chembe hai ya
mnyama au mmea
49
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 49 14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 49