Page 52 - SayansiStd4
P. 52
4. Baada ya masaa 24, chunguza kwa makini jinsi mayai
yalivyobadilika kuwa lava.
5. Endelea kuchunguza mara kwa mara kwa makini jinsi
FOR ONLINE READING ONLY
lava alivyobadilika na kuwa buu kwa kuongozwa na
maswali yafuatayo:
(a) Je, viumbe hivyo vimefunikwa na gamba lenye sifa
zipi?
(b) Je, viumbe hivyo vimebadilika baada ya siku ngapi?
(c) Je, viumbe hivyo vinajongea?
6. Hesabu mabuu kumi na uyabakize kwenye sahani.
7. Funika sahani hiyo kwa karatasi ya plastiki iliyotobolewa
vitobo vidogovidogo kwa kutumia pini.
8. Endelea kuchunguza mabuu kisha andika unachokiona
kwa kuongozwa na maswali yafuatayo:
(a) Je, ni mabuu mangapi yaliyobaki kwenye sahani?
(b) Je, nini kimetokea kwa mabuu mengine?
(c) Je, umeviona viumbe gani vingine kwenye sahani?
Kazi ya kufanya namba 4
Kuchunguza hatua za ukuaji wa mbu
Mahitaji: Lenzi ya mkononi, maji yaliyotuama kwa mda mrefu,
chupa au kifuu cha nazi na wavu wenye matundu
madogo
45
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 45
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 45 14/01/2025 18:39