Page 57 - SayansiStd4
P. 57
Sura ya Tatu
Maada
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Mazingira yanahusisha vitu vyenye uzito na vinavyochukua
nafasi. Vitu hivyo huitwa maada. Katika sura hii, utajifunza
hali za maada. Pia, utafanya majaribio sahili ya kuchunguza
hali zake. Umahiri utakaoujenga utakuwezesha kutumia
maada mbalimbali katika maisha ya kila siku.
Kuhusu vitu mbalimbali vyenye uzito
Fikiri
na vinavyochukua nafasi
Dhana ya maada
Maada ni kitu chochote chenye uzito na kinachochukua nafasi.
Mfano wa maada ni kama vile jiwe, maji na hewa.
Kazi ya kufanya namba 1
1. Tumia maktaba, matini mtandao au vyanzo vingine
kutafuta taarifa kuhusu dhana ya maada. kisha toa
mifano mingine ya maada.
2. Kusanya vitu mbalimbali, chunguza sifa zake, na uviweke
kwenye makundi kulingana na hali za maada kama vile
yabisi, kimiminika na gesi.
50
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 50
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 50 14/01/2025 18:39