Page 60 - SayansiStd4
P. 60
Zingatia: Hakikisha barafu imetokana na maji safi na salama.
Hatua
1. Chukua kipande kimoja cha barafu weka kwenye sufuria.
FOR ONLINE READING ONLY
Chunguza rangi ya barafu, bonyeza kwa vidole. Je,
imebonyea?
2. Chukua kipande kingine cha barafu, weka kwenye
sufuria kisha chunguza umbo lake. Weka barafu hiyo
kwenye jagi na uchunguze umbo lake baada ya muda
mfupi. Je, umbo na ukubwa wa barafu ulibadilika baada
ya kuwekwa kwenye jagi?
3. Washa jiko, kisha weka jikoni sufuria yenye kipande
kingine cha barafu. Je, umebaini nini?
4. Toa barafu nyingine ndani ya deli weka kwenye maji
yaliyoyeyuka. Je, umebaini nini?
5. Rekodi matokeo ya vitendo ulivyofanya katika kila hatua.
6. Chukua kipande cha barafu kutoka kwenye deli na
ukiweke juu ya uso ulionyooka, kama sinia. Inamisha
meza taratibu na chunguza matokeo. Je, barafu inatiririka
kama maji?
Matokeo
Maji katika hali ya yabisi (barafu) hayana rangi, hayabonyei,
umbo lake halibadiliki kuendana na chombo ilimowekwa, na
hayatiririki kama maji katika hali ya kimiminika. Barafu inaelea
juu ya kimiminika (maji), na inapokutana na hali ya joto,
huyeyuka na kuwa maji katika hali ya kimiminika.
Hitimisho
Maji katika hali ya yabisi (barafu) yanakuwa katika hali ya
uimara na ngumu, yana umbo na ujazo maalum, na hayana
uwezo wa kutiririka kama kimiminika (maji).
53
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 53
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 53 14/01/2025 18:39