Page 65 - SayansiStd4
P. 65
sentigredi 0 (nyuzijoto farenhaiti 32), barafu huyeyuka polepole
na kuwa kimiminika. Katika jotoridi nyuzijoto sentigredi 100, maji
huchemka na kuwa mvuke. Mvuke ukikutana na uso wenye
jotoridi la chini, hubadilika kuwa kimiminika tena. Mfano, mvuke
FOR ONLINE READING ONLY
unaotoka kwenye mdomo wa birika yenye maji yanayochemka
unakuwa wa moto na katika hali ya gesi. Gesi hiyo inapokutana
na kioo chenye jotoridi dogo hupoozwa na kuonekana kama
ukungu. Ukungu huu huendelea kupoozwa na kuwa katika hali
ya kimiminika. Hii inaonesha kuwa gesi ikipoozwa hubadilika
na kuwa kimiminika. Kitendo hiki huitwa utoneshaji. Hivyo,
utoneshaji ni mchakato wa kubadilisha hali ya gesi kwenda
kimiminika.
Zoezi namba 1
1. Maada ni nini?
2. Taja mifano miwili kwa kila hali ya maada na eleza
matumizi yake katika maisha yetu ya kila siku.
3. Kwa kuzingatia umbo na ujazo, yabisi inatofautiana vipi
na kimiminika na gesi?
4. Kwa jinsi gani maji yanaweza kupatikana katika hali tatu
za maada?
Kizingiti cha mgando wa maji
Maji huganda yanapofikia jotoridi maalumu. Kizingiti cha
mgando wa maji ni jotoridi maalumu ambapo kimiminika (maji)
huganda na kubadilika kuwa yabisi (barafu). Maji katika hali
yabisi (barafu) yana matumizi mengi kama, kuhifadhi vyakula
na vinywaji.
58
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 58
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 58 14/01/2025 18:39