Page 68 - SayansiStd4
P. 68
Jaribio namba 6: Kuchunguza kizingiti cha mchemko wa
maji
Lengo: Kuonesha kizingiti cha mchemko wa maji
FOR ONLINE READING ONLY
Mahitaji: Chanzo cha moto (jiko), maji, sufuria na
kipimajoto
Zingatia: Usitoe kipimajoto nje ya maji wakati unasoma
jotoridi la maji
Hatua
1. Weka sufuria yenye maji kwenye jiko lenye moto.
2. Pima jotoridi la maji yanapoanza kuchemka.
3. Endelea kupima jotoridi la maji hadi maji yanapochemka
kwa kasi.
4. Rekodi matokeo ya jotoridi la maji ulilopima.
Matokeo
Maji yanapofikia jotoridi la nyuzijoto sentigredi 100 (nyuzijoto
farenhaiti 212), huchemka. Jotoridi hilo linajulikana kama
kizingiti cha mchemko wa maji.
Hitimisho
Jaribio linathibitisha kwamba kizingiti cha mchemko wa maji
ni nyuzijoto sentigredi 100.
Zoezi la marudio
Sehemu A: Chagua jibu sahihi.
1. Kiwango cha jotoridi chini ya nyuzijoto sentigredi 0, maji
huwa katika hali ijulikanayo kama _____.
61
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 61
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 61 14/01/2025 18:39