Page 66 - SayansiStd4
P. 66
Jaribio namba 5: Kuchunguza kizingiti cha mgando wa maji
Lengo: Kuonesha kizingiti cha mgando wa maji
FOR ONLINE READING ONLY
Mahitaji: Jokofu, meza, kipimajoto, maji na kikombe cha
plastiki
Zingatia: Usitoe kipimajoto nje ya maji wakati ukiwa
unasoma jotoridi la maji.
Hatua
1. Weka kikombe cha plastiki chenye maji juu ya meza.
2. Tumbukiza kipimajoto ndani ya maji huku umeshikilia
kwa juu. Kielelezo namba 5 kinaonesha namna ya
kupima jotoridi la maji.
Kielelezo namba 5: Kupima jotoridi la maji
3. Soma jotoridi la maji. Hakikisha unapata msaada wa
kusoma jotoridi la maji hayo. Rekodi jotoridi.
4. Chukua maji ya kwenye kikombe weka kwenye jokofu
sehemu ya kugandishia. Pima jotoridi la maji kila baada
ya dakika 10.
59
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 59
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 59 14/01/2025 18:39