Page 62 - SayansiStd4
P. 62
Hitimisho
Jaribio linathibitisha kwamba maji katika hali yake ya
kimiminika hayana umbo maalum bali yanabaki na ujazo
FOR ONLINE READING ONLY
maalum.
Jaribio namba 3: Kuchunguza sifa za maji katika hali ya
gesi
Lengo: Kuonesha sifa za maji katika hali ya gesi
Mahitaji: Maji, sufuria, kioo, kipimajoto na chanzo cha
moto (jiko)
Zingatia: Kazi hii ifanyike chini ya uangalizi wa mwalimu
wa somo au mtaalamu wa maabara.
Hatua
1. Weka maji kwenye sufuria.
2. Washa jiko, kisha weka sufuria yenye maji kwenye jiko.
Acha maji yaanze kuchemka.
3. Chunguza unachokiona maji yanapoanza kuchemka.
4. Acha maji yachemke kwa muda wa dakika 10. Tumia
kipimajoto kupima jotoridi la maji hadi litakapofika
nyuzijoto sentigredi 100. Andika unachokiona?
5. Shikilia kioo juu ya mvuke unaotoka kwenye maji
yanayochemka. Unaona nini kwenye kioo?
6. Andika matokeo baada ya vitendo ulivyovifanya.
55
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 55
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 55 14/01/2025 18:39