Page 58 - SayansiStd4
P. 58
Hali za maada
Zipo hali mbalimbali za maada. Katika sehemu hii utajifunza
hali tatu za maada ambazo ni yabisi, kimiminika na gesi.
FOR ONLINE READING ONLY
Yabisi
Aina hii ya maada huwa imara na ngumu. Yabisi ina umbo
maalumu. Mawe, sufuria na kuni ni mifano ya vitu yabisi.
Kielelezo namba 1 kinaonesha mifano ya vitu yabisi.
Mawe Sufuria Kuni
Kielelezo namba 1: Mifano ya vitu yabisi
Kimiminika
Kimiminika hakina umbo maalumu
bali huendana na kifaa au chombo
kilimowekwa. Ukimimina maji kwenye
kifaa, maji yanachukua nafasi na
kuendana na umbo la kifaa hicho.
Mifano mingine ya kimiminika
inahusisha vitu mbalimbali ikiwemo
maji, juisi na soda. Kielelezo namba
2 kinaonesha kimiminika kikimiminwa
kwenye glasi.
Kielelezo namba 2: Kimiminika
kikimiminwa kwenye glasi
51
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 51
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 51 14/01/2025 18:39