Page 61 - SayansiStd4
P. 61
Jaribio namba 2: Kuchunguza sifa za maji katika hali ya
kimiminika
Lengo: Kuonesha sifa ya maji katika hali ya kimiminika
FOR ONLINE READING ONLY
Mahitaji: Jagi, sufuria, maji safi na salama, mfuko wa plastiki
na kikombe safi
Hatua
1. Mimina maji kwenye kikombe safi, kisha nusa na onja.
Je, umegundua nini?
2. Chunguza rangi ya maji. Je, umeona rangi gani?
3. Chukua maji, weka kwenye jagi na sufuria. Mengine
weka kwenye mfuko wa plastiki na uufunge.
4. Chunguza umbo la maji yakiwa kwenye jagi, sufuria na
mfuko wa plastiki.
5. Inamisha jagi au sufuria ili uone jinsi maji yanavyotiririka.
6. Mimina maji kutoka kwenye jagi kwenda kwenye kikombe
cha plastiki na uangalie ujazo wake. Kisha, mimina
maji kutoka kwenye mfuko wa plastiki kwenda kwenye
kikombe cha plastiki na linganisha ujazo na kiasi cha
awali kilichokuwa kwenye kikombe.
7. Rekodi matokeo ya vitendo ulivyovifanya.
Matokeo
Maji katika hali ya kimiminika hayana rangi, ladha wala harufu.
Hayana umbo maalum, bali huchukua umbo la chombo
yalimowekwa huku yakibaki na ujazo wake bila kujali chombo
hicho. Aidha, maji hutiririka kwa uhuru kutoka sehemu moja
hadi nyingine.
54
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 54
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 54 14/01/2025 18:39