Page 54 - SayansiStd4
P. 54
Mende hutaga mayai yaliyo katika sega gumu. Huficha mayai
yake kwenye sehemu zisizoonekana kwa urahisi. Baada ya
mwezi, mayai huanguliwa na kuwa tunutu. Tunutu ni mdogo
kimaumbile na huwa na ngozi laini, na hana mabawa. Baada
FOR ONLINE READING ONLY
ya miezi mitatu tunutu hubadilika na kuwa mende kamili.
Kielelezo namba 7 kinaonesha hatua za ukuaji wa mende.
Yai
Mende
Tunutu
Kielelezo namba 7: Hatua za ukuaji wa mende
Kufanya usafi mara kwa mara na kupanga vizuri nguo, vitabu
na vifaa mbalimbali itaondoa kabisa makazi na mazalia ya
mende. Vilevile, mende huangamizwa kwa kutumia sumu ya
kuua wadudu.
Zoezi la marudio
Sehemu A
1. Oanisha ugonjwa kutoka Sehemu A na dalili za ugonjwa
kutoka Sehemu B.
47
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 47 14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 47