Page 49 - SayansiStd4
P. 49
kusababishwa na mazingira. Mzio unaotokana na baadhi ya
vitu katika mazingira huchochea pumu kuanza. Vitu hivyo ni
kama vile moshi, vumbi, harufu ya manukato au sabuni na
chavua za maua. Vitu hivyo husababisha kuvimba na kujaa ute
FOR ONLINE READING ONLY
mzito katika kuta za ndani za njia ya hewa. Hali hii inapotokea
huzifanya njia hizo kuwa nyembamba. Njia za kupitisha
hewa zinapokuwa nyembamba hupunguza kiasi cha hewa
kinachoingia na kutoka na kufanya pumzi kubana.
Dalili za pumu
Dalili za ugonjwa wa pumu ni kama zifuatazo:
(a) Kukohoa, kupiga chafya na mafua;
(b) Kubanwa na kuumwa kifua na mbavu; na
(c) Pumzi kubana kunakoambatana na sauti kama filimbi au
mluzi.
Namna ya kuzuia pumu
Pumu ni hali ya kudumu ambayo haina tiba. Ugonjwa huu
unaweza kuzuiwa kwa:
(a) Kuepuka vichochezi vya pumu mfano chavua na manukato;
na
(b) Kupata matibabu ya kutuliza pumu mapema pindi dalili za
awali zinapojitokeza.
42
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 42 14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 42