Page 45 - SayansiStd4
P. 45
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 5: Mgonjwa anayeongezewa damu salama
(c) Maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Mtoto
anaweza kupata VVU kutoka kwa mama anayeishi na
VVU hasa wakati wa kujifungua. Vilevile, mtoto anaweza
kupata VVU kutoka kwa mama anayeishi na VVU wakati
wa kunyonya.
(d) Kufanya ngono na mtu mwenye VVU. Watoto hawatakiwi
kujihusisha na vitendo vya ngono. Vilevile, wasipite na
kucheza maeneo hatarishi yenye vishawishi vya kubakwa.
Maeneo hayo ni kama vile vilabu vya pombe na kumbi za
starehe. Maeneo mengine ni kama vile magofu ya nyumba
na vibanda vya kuoneshea sinema. Aidha, ni muhimu
kutoa taarifa kwa wazazi au walimu mapema endapo mtu
yeyote ataonesha dalili za kutaka kukufanyia vitendo vya
ngono ili kupata msaada sahihi.
Namna ya kuzuia maambukizi ya VVU na UKIMWI
VVU ni hatari na havina chanjo wala tiba. Hata hivyo, mtu
38
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 38
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 38 14/01/2025 18:39