Page 41 - SayansiStd4
P. 41
kutumia vyoo kwa usahihi. Tunapaswa kunawa mikono kwa
maji safi yanayotiririka na sabuni baada ya kutoka chooni na
kabla ya kula chakula. Mtu akipatwa na kipindupindu apelekwe
hospitali haraka au katika kituo maalumu kilichotengwa kwa
FOR ONLINE READING ONLY
ajili ya ugonjwa huo.
Zoezi namba 3
1. Eleza jinsi ugonjwa wa kipindupindu unavyoweza kuenea.
2. Unawezaje kumtambua mtu mwenye kipindupindu?
3. Ni mambo gani ya kufanya ili kuzuia kipindupindu?
4. Eleza kwa nini ni muhimu kunawa mikono yako kwa
sabuni na maji safi yanayotiririka baada ya kutumia choo.
Tetekuwanga
Tetekuwanga ni ugonjwa unaosababishwa na virusi. Ugonjwa
huu huambukizwa kwa njia ya kugusana mwili na mtu aliye na
tetekuwanga. Pia, huweza kuambukizwa kwa kuvaliana nguo
na mtu aliye na tetekuwanga.
Dalili za tetekuwanga
Dalili za tetekuwanga ni pamoja
na homa kali na kuumwa kichwa.
Vilevile, kutokwa na vipele
vinavyowasha ambavyo hubadilika
kuwa malengelenge yanayotoa
usaha au majimaji. Wakati
mwingine ugonjwa huu huacha
makovu ya kudumu kwenye ngozi.
Kielelezo namba 3 kinaonesha
mgonjwa wa tetekuwanga. Kielelezo namba 3:
Mgonjwa wa tetekuwanga
34
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 34
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 34 14/01/2025 18:39