Page 39 - SayansiStd4
P. 39
(d) Viungo vya mwili kukosa nguvu;
(e) Kutapika; na
(f) Kupoteza hamu ya kula.
FOR ONLINE READING ONLY
Namna ya kuzuia malaria
Ugonjwa wa malaria huzuiwa kwa kuharibu mazalia ya mbu.
Mazalia ya mbu ni kama vile kwenye vichaka, nyasi ndefu
na maji yaliyotuama kwenye vidimbwi. Pia, matairi, vifuu vya
nazi na makopo yaliyohifadhi maji yanaweza kuwa mazalia
ya mbu. Maji yaliyotuama yanaweza kumwagiwa mafuta ya
taa au viuadudu ili kuua mazalia ya mbu. Pia, vifuu vya nazi
na vifaa vingine vyenye mazalia vichomwe moto. Aidha, njia
za kujikinga na malaria ni kutumia vyandarua vyenye dawa
maalumu wakati wa kulala na kutumia dawa za kufukuza au
kuua mbu. Njia nyingine ya kujikinga na malaria ni kuweka
nyavu katika madirisha ya nyumba ili kuzuia mbu kuingia. Mtu
anapohisi dalili za malaria anapaswa kuwahi hospitali au katika
kituo cha afya ili apate uchunguzi na tiba sahihi.
Zoezi namba 2
1. Taja dalili nne za ugonjwa wa malaria.
2. Eleza umuhimu wa kulala kwenye chandarua.
3. Fafanua namna mtu anavyoweza kuambukizwa malaria.
4. Je, unawezaje kujikinga wewe na familia yako dhidi ya
malaria?
Kipindupindu
Kipindupindu ni ugonjwa unaosababishwa na bakteria.
Kipindupindu kinaenezwa kwa kula chakula au kunywa maji
yenye vimelea vya kipindupindu. Pia, ugonjwa huu huenezwa
32
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 32 14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 32