Page 37 - SayansiStd4
P. 37
Zoezi namba 1
1. Bainisha sehemu mbalimbali ambapo vimelea vya
magonjwa hupatikana.
FOR ONLINE READING ONLY
2. Eleza njia mbalimbali ambazo vimelea vya magonjwa
vinaweza kuingia mwilini mwa binadamu.
3. Taja magonjwa yoyote matatu unayoyafahamu katika
mazingira yako?
Aina za magonjwa
Kuna aina mbalimbali za magonjwa yanayoathiri utendaji
wa kawaida wa mwili wa binadamu. Magonjwa hayo
yamegawanyika katika makundi makuu mawili ambayo ni
magonjwa ya kuambukiza na yasiyoambukiza.
Kazi ya kufanya namba 1
1. Tumia maktaba, matini mtandao au vyanzo vingine
kutafuta taarifa kuhusu magonjwa ya kuambukiza na
yasiyo ya kuambukiza.
2. Orodhesha mifano mitano kwa kila kundi la magonjwa
uliyoyabaini.
Magonjwa ya kuambukiza
Magonjwa ya kuambukiza ni magonjwa yanayoenezwa
kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Magonjwa
hayo husababishwa na vimelea. Mfano wa vimelea hivyo ni
bakteria, na virusi. Magonjwa hayo ni kama vile kipindupindu,
tetekuwanga, kifua kikuu, homa ya ini na Ugonjwa wa Virusi vya
30
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 30
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 30 14/01/2025 18:39