Page 40 - SayansiStd4
P. 40
na nzi. Nzi anaweza kubeba vimelea kutoka kwenye matapishi
au kinyesi chenye vimelea kwenda kwenye chakula au maji.
Kielelezo namba 2 kinaonesha uenezwaji wa ugonjwa wa
kipindupindu.
FOR ONLINE READING ONLY
Nzi aliyebeba vimelea
vya ugonjwa akielekea
kwenye chakula
Kinyesi chenye
vimelea vya
ugonjwa wa Mtu
kipindupindu aliyeambukizwa
ugonjwa wa
kipindupindu
Kielelezo namba 2: Uenezwaji wa ugonjwa wa kipindupindu
Dalili za kipindupindu
Zifuatazo ni dalili za ugonjwa wa kipindupindu:
(a) Kuharisha na kutapika mfululizo;
(b) Kutoa kinyesi chenye rangi kama ya maji yaliyosafishiwa
mchele;
(c) Mkojo kuwa na rangi ya manjano; na
(d) Kulegea mwili na kuishiwa nguvu.
Namna ya kuzuia kipindupindu
Tunapaswa kuishi katika mazingira safi na kudumisha usafi.
Tunashauriwa kula chakula na kunywa maji safi na salama.
Aidha, ni muhimu kutumia choo wakati wa kujisaidia. Pia,
33
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 33 14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 33