Page 42 - SayansiStd4
P. 42
Namna ya kuzuia tetekuwanga
Tetekuwanga huzuiwa kwa kutochangia mavazi na kuzingatia
usafi wa mwili na mavazi kwa mgonjwa. Vilevile, dawa ya kuua
vimelea vya magonjwa itumike wakati wa kusafisha mwili na
FOR ONLINE READING ONLY
kufua nguo. Aidha, tetekuwanga huzuiwa kwa chanjo.
Zoezi namba 4
1. Eleza namna ambavyo tetekuwanga inaweza kuenea
kutoka kwa mtu mmoja hadi mwingine.
2. Unawezaje kutambua kama mtu ana tetekuwanga?
3. Ni mambo gani unaweza kufanya ili kuzuia kuenea kwa
tetekuwanga?
Kifua kikuu
Ugonjwa wa kifua kikuu unasababishwa na bakteria. Ugonjwa
huu unaathiri zaidi mapafu. Hata hivyo, unaweza kuathiri
sehemu zingine za mwili kama vile uti wa mgongo, mifupa na
figo. Ugonjwa wa kifua kikuu huenezwa kwa njia ya hewa, hasa
mtu aliye na vimelea vya kifua kikuu akikohoa au kupiga chafya.
Pia, kutema mate ovyo husababisha vijidudu kusambaa. Hali
hii husababisha mtu mwingine kuambukizwa.
Dalili za kifua kikuu
Zifuatazo ni miongoni mwa dalili za ugonjwa wa kifua kikuu:
(a) Kukohoa mfululizo kwa muda wa wiki mbili au zaidi;
(b) Kupata maumivu ya kifua;
(c) Homa za usiku na kutoka jasho jingi usiku;
(d) Kupungua uzito ndani ya muda mfupi;
35
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 35
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 35 14/01/2025 18:39