Page 43 - SayansiStd4
P. 43
(e) Kukohoa damu; na
(f) Kukosa hamu ya kula chakula.
Namna ya kuzuia kifua kikuu
FOR ONLINE READING ONLY
Kifua kikuu hudhibitiwa kwa njia ya chanjo kwa watoto wachanga.
Njia nyingine za kuzuia ni pamoja na kuzingatia usafi wa mwili,
kuepuka msongamano wa watu. Pia, epuka kuchangia vyombo
na watu wenye maambukizi. Watu waliopata maambukizi ya
kifua kikuu hupatiwa dawa za kutibu ugonjwa huo chini ya
uangalizi wa mhudumu wa afya.
Zoezi namba 5
1. Eleza namna kukohoa, kupiga chafya, na kutema mate
kunavyoweza kuchangia kuenea kwa kifua kikuu.
2. Dalili gani zinaweza kukuwezesha kumtambua mtu
mwenye kifua kikuu?
3. Ni sehemu gani nyingine za mwili ambazo kifua kikuu
kinaweza kuathiri mbali na mapafu?
Virusi vya UKIMWI (VVU) na UKIMWI
UKIMWI husababishwa na Virusi vya UKIMWI (VVU). VVU
hushambulia chembe hai nyeupe za damu ambazo hujenga
kinga ya mwili. Chembe hai hizo zinaposhambuliwa na VVU
husababisha mwili kupoteza uwezo wa kujikinga dhidi ya vimelea
vya magonjwa. Virusi vya UKIMWI vinapozidi kuongezeka
hudhoofisha mwili na kusababisha kushambuliwa na magonjwa.
Udhaifu wa mwili na magonjwa huweza kusababisha kifo.
36
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 36
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 36 14/01/2025 18:39