Page 46 - SayansiStd4
P. 46
anayeishi na VVU anaweza kupata dawa za kupambana na VVU
ili kurefusha maisha na kuwa na afya. VVU vinaweza kuzuiwa
kwa kutochangia vitu kama miswaki na vifaa vyenye ncha kali.
Pia, kutojihusisha na vitendo vya ngono. Mtu anayeishi na VVU
FOR ONLINE READING ONLY
na mwenye UKIMWI anatakiwa kupata lishe bora na yenye mlo
kamili. Pia, anashauriwa kufanya mazoezi mara kwa mara.
Aidha, watu wanoishi na VVU wanapaswa kuoneshwa upendo,
kuthaminiwa na kutonyanyaswa.
Zoezi namba 6
1. Taja njia tatu zinazochangia maambukizi ya VVU.
2. Eleza jinsi gani vifaa vyenye ncha kali vinaweza kuchangia
maambukizi ya VVU.
3. VVU huathiri kinga ya mwili kwa namna gani?
4. Eleza unavyoweza kuwajali na kuwasaidia waishio na
VVU.
Magonjwa yasiyoambukiza
Magonjwa yasiyoambukiza ni yale yasiyoenezwa kutoka kwa
mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Vilevile, hayasababishwi
na vimelea. Magonjwa hayo yanaweza kuwa ya kurithi kutoka
kizazi kimoja kwenda kingine. Aidha, huweza kusababishwa na
mtindo wa maisha usio sahihi. Magonjwa yasiyoambukiza ni
kama vile saratani, kisukari na pumu.
Saratani
Saratani ni ugonjwa ambao hutokea kwenye chembe hai za
mwili. Chembe hai hizo huanza kujigawa na kutengeneza
chembe hai mpya bila mpangilio maalumu. Chembe hai
huendelea kukua kwa kasi na kutengeneza uvimbe. Uvimbe au
chembe hai zenye hitilafu huitwa saratani na huweza kutokea
39
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 39 14/01/2025 18:39