Page 44 - SayansiStd4
P. 44
Njia za maambukizi ya VVU
VVU vinakaa kwenye majimaji ya mwili wa binadamu hasa
damu. VVU huambukizwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa
mwingine kwa njia mbalimbali kama vile zifuatazo:
FOR ONLINE READING ONLY
(a) Kuchangia mswaki na vifaa vyenye ncha kali kama
sindano, wembe, hereni, pini na mkasi. Kuchangia
vifaa vyenye ncha kali na mtu mwenye VVU kunaweza
kusababisha maambukizi. Kielelezo namba 4 kinaonesha
vifaa vinavyoweza kuchangia maambukizi ya VVU.
Kielelezo namba 4: Vifaa vinavyoweza kuchangia maambukizi ya VVU
(b) Kuongezewa damu yenye VVU. Kuongezewa damu yenye
VVU kunasababisha maambukizi. Damu ni lazima ipimwe
na kuhakikiwa kuwa ipo salama na kuwa haina VVU kabla
ya kumwongezea mgonjwa. Kielelezo namba 5 kinaonesha
mgonjwa anayeongezewa damu salama katika kituo cha
afya.
37
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 37
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 37 14/01/2025 18:39