Page 47 - SayansiStd4
P. 47
sehemu yoyote ya mwili kama vile kwenye damu, utumbo,
ubongo na mifupa.
Visababishi vya saratani
FOR ONLINE READING ONLY
Saratani husababishwa na vitu mbalimbali vinavyoharibu
mpangilio wa chembe hai za mwili. Vitu hivyo ni kama vile mionzi
mikali na kemikali kutoka kwenye vyakula, hewa, vipodozi au
dawa tunazotumia.
Namna ya kuzuia saratani
Ugonjwa wa saratani unaweza kuzuiwa kwa kujiepusha na ulaji
wa vyakula na vinywaji vyenye kemikali na matumizi holela ya
vipodozi na dawa. Vilevile, kujiepusha na unywaji wa pombe
na uvutaji wa sigara. Unywaji wa pombe na uvutaji wa sigara
huchochea saratani. Ugonjwa wa saratani unaweza kutibika
ikiwa mgonjwa atapelekwa hospitali mapema kwa ajili ya
uchunguzi.
Kazi ya kufanya namba 2
1. Tumia maktaba, matini mtandao na vyanzo vingine
kutafuta taarifa kuhusu aina mbalimbali za saratani.
2. Bainisha aina za saratani zinazopatikana zaidi nchini
Tanzania.
Kisukari
Ugonjwa wa kisukari husababishwa na mwili kushindwa kudhibiti
kiwango cha sukari kwenye damu. Ugonjwa huu hutokea
endapo tezi ya kongosho itashindwa kutengeneza homoni ya
insulini ya kutosha. Homoni ya insulini husaidia kurekebisha
kiwango cha sukari kwenye damu. Mtu huweza kuzaliwa na
ugonjwa wa kisukari kwa kurithi kutoka kwa wazazi.
40
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 40 14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 40