Page 48 - SayansiStd4
P. 48
Dalili za kisukari
Zifuatazo ni miongoni mwa dalili za kisukari:
(a) Kukojoa mara kwa mara;
FOR ONLINE READING ONLY
(b) Kupungua uzito kwa haraka;
(c) Kuwa na kiu isiyoisha hata kama utakunywa maji ya
kutosha;
(d) Uchovu wa mwili;
(e) Kutoona vizuri;
(f) Vidonda visivyopona haraka; na
(g) Kupata ganzi mikononi au miguuni.
Namna ya kuzuia kisukari
Ugonjwa wa kisukari unaweza kudhibitiwa kwa kufuata kanuni
za afya bora. Kanuni hizo ni pamoja na ulaji sahihi na kudhibiti
ongezeko la uzito wa mwili. Tunashauriwa kufanya mazoezi ya
mwili mara kwa mara ili kupunguza hatari ya kupata kisukari.
Zoezi namba 7
1. Taja dalili tatu zinazokuwezesha kutambua kuwa mtu
ana ugonjwa wa kisukari.
2. Kwa nini mazoezi ya mwili ya mara kwa mara yanaweza
kusaidia kuzuia ugonjwa wa kisukari?
3. Eleza kwa nini ulaji sahihi wa vyakula unaweza kuzuia
ugonjwa wa kisukari.
Pumu
Pumu ni aina ya ugonjwa unaoathiri mfumo wa upumuaji.
Ugonjwa wa pumu unaweza kurithiwa kutoka kwa wazazi au
41
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 41 14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 41