Page 50 - SayansiStd4
P. 50
Zoezi namba 8
1. Fafanua namna mtindo wa maisha unavyoweza
kusababisha ugonjwa wa kisukari.
FOR ONLINE READING ONLY
2. Orodhesha vichochezi vyovyote vitatu vya ugonjwa wa
pumu.
3. Fafanua namna unavyoweza kuepuka ugonjwa wa
saratani.
Ukuaji wa wadudu wanaoeneza magonjwa
Wadudu hueneza baadhi ya magonjwa kwa binadamu. Mfano
wa wadudu wanaoeneza magonjwa ni kama vile nzi, mbu
na mende. Ukuaji wa wadudu hao hufuata hatua maalumu
hadi kutokea kwa mdudu kamili. Wakati wa ukuaji wadudu
hubadilika umbo na tabia, hatua hii huitwa metamofosisi. Kuna
aina mbili za metamofosisi ambazo ni metamofosisi kamili na
metamofosisi pungufu.
Metamofosisi kamili inahusisha hatua nne za ukuaji wa mdudu.
Hatua hizo ni yai, lava, buu na mdudu kamili. Wadudu kama vile
nzi na mbu wana metamofosisi kamili. Metamofosisi pungufu
inahusisha hatua tatu za ukuaji. Hatua hizo ni yai, tunutu na
mdudu kamili. Metamofosisi hii hutokea kwa wadudu kama vile
mende na chawa.
Hatua za ukuaji wa nzi
Hatua za ukuaji wa nzi ni yai, lava, buu na nzi kamili. Nzi
jike hutaga mayai katika mazingira machafu ambapo hupata
chakula chake. Mazingira hayo ni kama vile sehemu zenye
vinyesi, mabaki ya chakula na mizoga. Mayai ya nzi huanguliwa
na kuwa lava ndani ya masaa ishirini na nne. Hii hutegemea
hali ya mazingira kama vile joto. Lava anatumia angalau siku
43
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 43
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 43 14/01/2025 18:39