Page 38 - SayansiStd4
P. 38
Korona (UVIKO-19). Baadhi ya magonjwa yanayoambukiza ni
kama yafuatayo:
Malaria
FOR ONLINE READING ONLY
Malaria ni ugonjwa unaosababishwa na vimelea viitwavyo
plasmodium. Ugonjwa huu huenezwa na mbu jike anayeitwa
anofelesi. Mbu huyo huambukiza malaria kwa kuingiza vimelea
vya ugonjwa mwilini anapomuuma mtu. Kielelezo namba 1
kinaonesha uenezwaji wa ugonjwa wa malaria.
Mtoto akiambukizwa
malaria
Mtu mzima
akiambukizwa
malaria
Mtu mwenye
maambukizi ya malaria
Kielelezo namba 1: Uenezwaji wa ugonjwa wa malaria
Dalili za malaria
Miongoni mwa dalili za ugonjwa wa malaria ni kama vile:
(a) Homa kali inayoambatana na kupanda kwa joto mwilini;
(b) Kuhisi baridi na kutetemeka mwili;
(c) Kuumwa kichwa;
31
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 31 14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 31