Page 36 - SayansiStd4
P. 36
Sura ya Pili
Magonjwa
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Magonjwa huathiri afya za watu. Katika sura hii, utajifunza
kuhusu magonjwa ya binadamu. Aidha, utajifunza njia za
maambukizi, visababishi na namna ya kudhibiti na kujikinga
na magonjwa. Vilevile, utajifunza hatua za ukuaji wa baadhi
ya wadudu wanaoeneza magonjwa mbalimbali. Umahiri
utakaoujenga utakuwezesha kudhibiti magonjwa mbalimbali.
Vilevile, kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya magonjwa.
Madhara ya magonjwa katika afya ya
Fikiri
binadamu
Dhana ya magonjwa
Ugonjwa ni hali ambayo inadhoofisha afya na hivyo kuathiri
utendaji wa kawaida wa mwili. Magonjwa mengi hutokana
na vimelea au vijidudu mbalimbali vilivyopo katika mazingira
yetu. Vimelea hivyo huishi katika hewa, udongo, maji, chakula
kisicho salama na kwenye majimaji ya miili ya wanyama kama
vile damu. Vimelea hivyo huingia mwilini kupitia njia mbalimbali
kama vile kula chakula chenye vimelea, kuvuta hewa na
kugusana. Aidha, baadhi ya magonjwa hayatokani na vimelea.
Magonjwa hayo ni kama vile magonjwa ya kurithi.
29
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 29
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 29 14/01/2025 18:39