Page 73 - Sayansi_Drs_4
P. 73
uunguaji wa vitu hutumika katika kazi nyingi kama vile kupika
chakula, kuyeyusha chuma, na kuchoma taka.
Kazi ya kufanya namba 1
FOR ONLINE READING ONLY
1. Tumia maktaba, matini mtandao au vyanzo vingine vya
taarifa kubainisha mahitaji muhimu ya kuungua kwa vitu.
2. Eleza uunguaji uliowahi kusimuliwa au kuushuhudia
katika mazingira unayoishi.
Mahitaji muhimu ili uunguaji uweze kutokea
Ili uunguaji uweze kutokea vinahitajika vitu vitatu ambavyo ni
joto, gesi ya oksijeni na vitu vinavyoweza kuungua (fueli).
Joto
Joto hupandisha kiwango cha jotoridi la fueli. Ili uunguaji
uanze, ni lazima kuwe na joto la kutosha kuunguza vitu. Joto
hili linaweza kutoka kwenye cheche za moto, kijinga cha moto,
au kitu kingine kinachotoa joto.
Oksijeni
Oksijeni ni gesi inayohitajika ili uunguaji wa vitu uweze kutokea.
Oksijeni ikikosekana, uunguaji wa vitu hauwezi kutokea.
Fueli
Fueli inaweza kuwa katika hali ya yabisi, kimiminika au gesi.
Mfano wa fueli ni kama kuni, mkaa, gesi, mafuta au vitu vingine
vinavyoweza kushika moto na kuungua.
Uhusiano wa gesi ya oksijeni, joto na fueli huunda pembetatu
ya moto kama inavyooneshwa katika Kielelezo namba 1.
66
05/11/2024 14:50
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 66
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 66 05/11/2024 14:50