Page 74 - Sayansi_Drs_4
P. 74
Hivyo, kitu kimojawapo kikikosekana uunguaji wa vitu hauwezi
kutokea.
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 1: Pembetatu ya moto
Umuhimu wa gesi ya oksijeni katika uunguaji wa vitu
Jaribio namba 1: Kuchunguza umuhimu wa gesi ya oksijeni
katika uunguaji.
Lengo: Kuonesha umuhimu wa hewa ya oksijeni katika
uunguaji wa vitu
Mahitaji: Kiberiti, mishumaa miwili, chombo angavu
chenye uwazi upande mmoja au jagi lenye
kuzuia hewa kupita, saa na meza
Hatua
1. Chukua mishumaa miwili kisha iwekee alama A na B.
2. Chukua kiberiti na uwashe mishumaa yote miwili.
3. Funika mshumaa B kwa kutumia chombo angavu chenye
uwazi upande mmoja kuzuia hewa isipite
67
05/11/2024 14:50
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 67
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 67 05/11/2024 14:50