Page 72 - Sayansi_Drs_4
P. 72
Sura ya Nne
Uunguaji wa vitu
FOR ONLINE READING ONLY
Utangulizi
Uunguaji wa vitu hutokea katika maisha ya kila siku. Katika
sura hii, utajifunza maana, sababu, na athari za uunguaji
wa vitu. Pia, utajifunza mbinu mbalimbali za kujilinda na
ajali zinazoweza kutokea kutokana na kuungua kwa vitu.
Pia, utafanya majaribio sahili ya kuchunguza umuhimu wa
hewa (gesi ya oksijeni) katika uunguaji wa vitu. Umahiri
utakaoujenga utakuwezesha kuzalisha joto na mwanga kwa
usalama kwa ajili ya matumizi mbalimbali. Vilevile, utaweza
kujikinga na kuwakinga wengine na ajali zitokanazo na
kuungua kwa vitu.
Kuhusu umuhimu na athari za uunguaji
Fikiri
wa vitu katika maisha ya kila siku
Dhana ya uunguaji wa vitu
Uunguaji wa vitu ni mchakato unaotokea wakati vitu vyenye
uwezo wa kuungua (Fueli) vinaungana na gesi ya oksijeni na
kutoa joto na mwanga. Wakati wa mchakato wa uunguaji wa
vitu, nishati hutolewa kwa njia ya joto na mwanga, ndiyo sababu
unaona miali ya moto na kuhisi joto wakati kitu kinawaka. Kwa
mfano, unapounguza kuni kwenye moto, kuni zinachanganyika
na gesi ya oksijeni, na kutoa joto na mwanga. Mchakato huu wa
65
05/11/2024 14:50
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 65
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 65 05/11/2024 14:50