Page 78 - SayansiStd4
P. 78
Utengenezaji wa mkaa ni mfano wa uunguaji usio kamili;
kuni zinapochomwa kwenye tanuri lililofunikwa na udongo,
hubadilika kuwa mkaa kutokana na upungufu wa oksijeni.
FOR ONLINE READING ONLY
Hitimisho
Jaribio linaonesha uunguaji usio kamili uliosababishwa
na ukosefu wa oksijeni ya kutosha, na kusababisha mkaa
kutokuungua kabisa.
Katika Jaribio namba 2 kuni zinaungua na kutoa joto na
mwanga. Kuni zote zinaungua kabisa na kuwa majivu. Hii ni
kwa sababu tukio la uunguaji linafanyika katika uwepo wa
oksijeni ya kutosha. Katika jaribio namba 3, uunguaji ulifanyika
katika kiwango kidogo cha oksijeni. Hii ilisababisha utoaji wa
joto kidogo bila mwanga. Kuni ziligeuka kuwa mkaa badala ya
kuungua kabisa.
Matokeo ya kuungua kwa vitu
Kuungua kwa vitu huweza kusababisha matokeo mbalimbali
yanayoweza kuwa na faida au hasara kwa viumbe hai na
mazingira.
Faida za kuungua kwa vitu
Zifuatazo ni baadhi ya faida za kuungua kwa vitu:
(a) Kuzalisha nishati inayotumika katika kupika, kupasha joto,
na kuendesha mitambo mbalimbali. Kwa mfano, kuungua
kwa gesi kwenye majiko hutoa nishati ya kupika chakula.
Kielelezo namba 2 kinaonesha shughuli za mapishi;
71
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 71
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 71 14/01/2025 18:39