Page 80 - SayansiStd4
P. 80

Hasara za kuungua kwa vitu

              Uunguaji  wa  vitu  huweza kusababisha  hasara mbalimbali.
              Miongoni wa hasara hizo ni:

          FOR ONLINE READING ONLY
              (a)  Uharibifu  mkubwa  wa mazingira  kwa kuharibu  uoto wa
                   asili na makazi ya wanyama;

              (b)  Mmomonyoko wa udongo na kupoteza rutuba ya ardhi
                   Uchomaji wa misitu unaweza kusababisha;


              (c)  Kuharibu majengo na vifaa mbalimbali vyenye thamani, na
                   kusababisha upotevu mkubwa wa mali. Kielelezo namba 4
                   kinaonesha uunguaji wa vitu; na

















                                    Kielelezo namba 4: Uunguaji wa vitu


              (d)  Kuungua kwa vitu kama vile mkaa na mafuta ya petroli,

                   huchangia ongezeko la gesi chafuzi angani.

              Kujilinda na kuungua

              Kujilinda  dhidi ya  ajali zinazohusisha  vitu  vinavyoungua,
              kunahitaji  mbinu mbalimbali  za kimaandalizi  na kiusalama.
              Zifuatazo ni mbinu ambazo zitakulinda wewe na wengine dhidi

              ya ajali zinazosababishwa na vitu vinavyoungua:

              Hifadhi vizuri vifaa vinavyolipuka

              Weka mbali na vyanzo vya joto na moto vitu vinavyoweza
              kulipuka (kama petroli, mafuta ya taa na kemikali);



                                                   73




                                                                                            14/01/2025   18:39
     SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd   73                                   14/01/2025   18:39
     SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd   73
   75   76   77   78   79   80   81   82   83   84   85