Page 85 - SayansiStd4
P. 85
likiwemo jua na radi. Pia, joto hutokana na vyanzo visivyo vya
asili kama vile moto wa kuni, mkaa, makaa ya mawe, umeme,
mafuta, msuguano na gesi. Vyanzo hivi vya joto hutumika
kuzalisha joto kwa matumizi mbalimbali ya kila siku. Chunguza
FOR ONLINE READING ONLY
Kielelezo namba 1, kisha soma maelezo yanayofuata.
(a) Jua (b) Jiko la kuni (c) Jiko la mkaa
(d) Jiko la umeme (e) Jiko la gesi
Kielelezo namba 1: Vyanzo vya nishati ya joto
Kielelezo namba 1(a) kinaonesha jua ambalo ni chanzo
kikuu asili cha nishati ya joto. Vielelezo namba 1(b) na 1(c)
vinaonesha vitendo vya kupika chakula kwa kutumia kuni na
mkaa. Vielelezo namba 1(d) na 1(e) vinaonesha vitendo vya
kupika chakula kwa kutumia umeme na gesi.
Kazi ya kufanya namba 1
Kubaini chanzo cha joto
Mahitaji: Kijiti kimoja kikavu na kipande cha mti kilichokauka
Hatua
1. Fikicha viganja vya mikono yako.
78
14/01/2025 18:39
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 78
SAYANSI DARASA LA IV KITABU CHA MWANAFUNZI.indd 78 14/01/2025 18:39